Thursday, February 23, 2017

VIDEO: Nje ya Mahakama kuu baada ya kesi ya Mbowe, Wema Sepetu pembeni

Tags


Kutoka Mahakama kuu Dar es salaam leo jioni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea baada ya kutoka Mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa DSM na Kamshna Sirro.
Tundu Lissu amewaambia Waandishi wa habari kwamba Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokua wanaweza kumuita kwa Mahojiano ambapo pia Mahakama itatoa maamuzi March 2 2017, zaidi unaweza kumtazama Tundu Lissu hapa chini..
Pamoja na hayo, Mwigizaji Wema Sepetu alikuwepo Mahakamani hapo toka asubuhi ambapo ameonekana jioni hii akiwa pembeni ya viongozi wa CHADEMA na baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA walionekana kumkaribishwa kwa maneno wakati akiingia kwenye gari, hii video hapa chini itakuonyesha
FULL VIDEO: Wema Sepetu pembeni ya Freeman Mbowe Mahakamani leo Dar es salaam, bonyeza hapa chini kutazama
VIDEO: “Unapotangaza mtu aje Polisi saa 5 wewe ni nani? – FREEMAN MBOWE…. Tazama hii video hapa chini kumuona akiongea


EmoticonEmoticon

Kichuyaaaaaaa: Tanzania 2 v DRC 0