Tuesday, February 28, 2017

VIDEO: Baada ya Wizara ya mambo ya nje kuhamia Dodoma wameyaongea haya

Tags


June 2016 Rais John Pombe Magufuli alitangaza kuwa ni lazima Serikali yake yote kuhamia Dodoma huku akiagiza Wizara zote hadi kufikia February 28 2017 awamu yote ya kwanza iwe tayari imehamia Dodoma, Leo February 27 2017 Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa A.Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ameongea na Waandishi wa habari baada ya kutekeleza agizo hilo.
Full video ya Waziri Mahiga nimekuwekea hapa chini alipokuwa akielezea…
VIDEO: Serikali imetaja makosa matatu yaliyofanywa na Watanzania wanaofukuzwa Msumbiji 

Monday, February 27, 2017

VIDEO: Makosa matatu yaliyofanywa na Watanzania waliofukuzwa Msumbiji

Tags


Bado ishu ya Watanzania kuondolewa kwenye nchi jirani ya Msumbiji ipo kwenye headlines ambapo leo February 27 2017 Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika  Mashariki Dr. Augustine Mahiga amezungumza Dodoma.
Waziri Mahiga ametaja baadhi ya sababu zilizopelekea Watanzania hao kufukuzwa na hapa ninamnukuu >>> “Watanzania walioondolewa Msumbiji wengi wao walikwenda kwa njia ambazo hata kwa Tanzania sio halali”
Kupata kila akichosema unaweza kubonyeza play kwenye hii video hapa chini kujionea

Baada ya Wizara ya Afya kuahirisha kutaja wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja TZ

Tags


Marko maluli
Leo February 27 2017 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilikua na mpango kuwa na Mkutano na Waandishi wa habari ulioandaliwa kuwataja Watanzania wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kujiuza mitandaoni lakini baadae leo Mkutano huo uliahirishwa.
Baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameandika kupitia account yake ya twitter haya……
“Kwa orodha tuliyonayo, kutangaza majina ya mashoga hadharani, ni sawa na kufungulia jini lililowekwa kwenye chupa!”-Kigwangalla
“Kwa sababu za kimkakati, na ili kuepuka kuharibu ushahidi, tutalishughulikia jambo hili kwa namna nyingine, tutawajulisha matokeo kila hatua”-Kigwangalla

FULL VIDEO: Waziri Lukuvi asema eneo alilopewa Paul Makonda lina utata

Tags


Marko maluli

Waziri wa ardhi William Lukuvi ameita Waandishi wa habari Dar es salaam February 27 2017 na kuongelea ishu ya Kiwanja alichopewa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda juzi na Mfanyabiashara mmoja ili akigawe bure kwa Wananchi kwa ajili ya kutengeneza Viwanda vidogovidogo.
Kila kitu pamoja na ishu nyingine ya Wizara ya ardhi kuhamia Dodoma utakutana nacho kwenye hii video hapa chini akiongea mwenyewe WaziriWilliam Lukuvi.

VIDEO: Simu Mstaafu Jakaya Kikwete aliyompigia Ridhiwani baada ya kuona picha yake na Lowassa

Tags


Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amepita kwenye OnAIR with Millard Ayona kuongelea ishu mbalimbali ikiwemo simu aliyopigiwa na Baba yake ambaye ni Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kuona ile picha aliyopiga na Edward Lowassa uwanja wa taifa Dar es salaam kwenye mechi ya Yanga vs Simba.
Ikiwa hii ni Part 1, pamoja na hiyo picha na Edward Lowassa ambayo imetawala mitandaoni weekend hii iliyoisha,Ridhiwani ameongelea ishu mbalimbali za Chalinze na game ya Yanga vs Simba iliyomalizika juzi kwa ushindi wa 1-2,tazama kila kitu kwenye hii video hapa chini

Friday, February 24, 2017

GLOBAL TV ONLINE - LIVE: Wema Sepetu Alivyorudisha Kadi ya CCM na Kujiun...

Tags

VIDEO: Polisi DSM yaongea, Sirro ajibu ya Freeman Mbowe na Steve Nyerere

Tags


Marko maluli
Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro leo February 24  2017 amekutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa kuhusu ukamataji wa Watuhumiwa wa dawa za kulevya, utumiaji na usambaji wa dawa za hizo ambapo amesema watuhumiwa 257 wamekamatwa kuanzia February 16 2017 mpaka February 23 2017.
Pamoja na hayo Kamanda Sirro amejibu maswali ya waandishi likiwamo kuhusu kumshikilia Mchekeshaji Steve Nyerere ambapo amesema……>>> kama ameitwa atakuwa ameitwa na wapelelezi sijapata habari zake, kwa kuwa kuna timu inashughulika na mambo haya
Hii video hapa chini ina kila kitu alichosema Simon Sirro leo, bonyeza play tu kumtazama

Ratiba ya 16 bora ya UEFA Europa League KRC Genk vs ? Man United vs ?

Tags


Marko maluli
Baada ya kumalizika kwa hatua ya 32 bora ya michuano ya UEFA Europa League, Ijumaa ya February 24 katika mji wa Stockholm Sweden ilichezeshwa droo ya kupanga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, timu ya KRC Genkinayochezewa na Mbwana Samattaimepangwa kucheza na wapinzania waoKAA Gent.
KRC Genk imepangwa kucheza na KAA Genk zikiwa na timu zote zinazotokaUbelgiji, hivyo ushindani wa game hiyo hautakuwa wa kawaida, Man Unitedwao wamepangwa na FC Rostov yaUrusi.
Hii ndio ratiba ya 16 bora ya michuano ya UEFA Europa League 2016/2017
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5

Thursday, February 23, 2017

VIDEO: Nje ya Mahakama kuu baada ya kesi ya Mbowe, Wema Sepetu pembeni

Tags


Kutoka Mahakama kuu Dar es salaam leo jioni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea baada ya kutoka Mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa DSM na Kamshna Sirro.
Tundu Lissu amewaambia Waandishi wa habari kwamba Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokua wanaweza kumuita kwa Mahojiano ambapo pia Mahakama itatoa maamuzi March 2 2017, zaidi unaweza kumtazama Tundu Lissu hapa chini..
Pamoja na hayo, Mwigizaji Wema Sepetu alikuwepo Mahakamani hapo toka asubuhi ambapo ameonekana jioni hii akiwa pembeni ya viongozi wa CHADEMA na baadhi ya Wafuasi wa CHADEMA walionekana kumkaribishwa kwa maneno wakati akiingia kwenye gari, hii video hapa chini itakuonyesha
FULL VIDEO: Wema Sepetu pembeni ya Freeman Mbowe Mahakamani leo Dar es salaam, bonyeza hapa chini kutazama
VIDEO: “Unapotangaza mtu aje Polisi saa 5 wewe ni nani? – FREEMAN MBOWE…. Tazama hii video hapa chini kumuona akiongea

FULL VIDEO: Wema Sepetu pembeni ya Freeman Mbowe Mahakamani

Tags


Mwigizaji Wema Sepetu ameungana na viongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mahakama kuu Dar es salaam Tanzania ambapo muda mfupi baada ya kuonekana pamoja, Msemaji wa CHADEMA amethibitisha kuwa wanatarajia kumtangaza kama Mwanachama mpya… 
TAZAMA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: Wema Sepetu alivyorudi Mahakamani jana February 22 2017, tazama kwenye hii video hapa chini
VIDEO: Irene Uwoya aongea kwanini hakupost wala kusema chochote Wema Sepetu alipokamatwa sakata la dawa za kulevya… PLAY HAPA CHINI

FULL VIDEO: Wema Sepetu pembeni ya Freeman Mbowe Mahakamani

Tags

Marko maluli
Mwigizaji Wema Sepetu ameungana na viongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mahakama kuu Dar es salaam Tanzania ambapo muda mfupi baada ya kuonekana pamoja, Msemaji wa CHADEMA amethibitisha kuwa wanatarajia kumtangaza kama Mwanachama mpya… 
TAZAMA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: Wema Sepetu alivyorudi Mahakamani jana February 22 2017, tazama kwenye hii video hapa chini
VIDEO: Irene Uwoya aongea kwanini hakupost wala kusema chochote Wema Sepetu alipokamatwa sakata la dawa za kulevya… PLAY HAPA CHINI

Ushauri wa waziri Nape kwa mashabiki wasio na uvumilivu Simba vs Yanga Feb 25 2017

Tags

Marko maluli


February 23 2017 wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuchangia Serengeti Boyswaziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Nape Moses Nnauyeamezungumzia kuhusu mashabiki wataokwenda kutazama mechi yaSimba na Yanga Jumamosi February 25 2017 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Waziri Nape amewashauri tu mashabiki ambao hawawezi kuwa na uvumilivu pale matokeo ya mechi yanapokuwa mabaya kwa upande wao “Jumamosi kuna mechi ya Simba na Yanga mtakumbuka mechi iliyopita kulikuwa na matatizo lakini nawaomba watanzania tuweke ustaarabu na uzalendo wetu mbele”
“Kama ukikasirika kunywa maji au nenda nyumbani tunaomba tusiharibu miundombinu ya uwanja, Simba wanajua gharama waliyotumia kukarabati uwanja ule, ukiona huna moyo wa kukaa uwanjani basi kaa nyumbani kwako angalia katika TV ukikasirika vunja TV yako”
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5

HEKAHEKA: Ndugu wapewa maiti isiyo ya ndugu yao na kuzua taharuki hospitalini Katavi

Tags


Marko maluli
Leo February 23 2017 kupitia hekaheka ya Leo tena ya Clouds FM, Mtangazaji Geah Habib ameileta inayotokea Katavi kuhusu ndugu waliopewa maiti ambayo si ya ndugu yao na kuambiwa kuwa ile ya ndugu yao imechanganywa na imeshazikwa na manispaa.
Kusikiliza full stori, Bonyeza play hapa chini
HEKAHEKA: Ndugu wapewa maiti isiyo ya ndugu yao na kuzua taharuki Katavi,Bonyeza play hapa chini

U-HEARD: "Huwezi ukaishi kimara ukajiita Rais wa Manzese"-Kitale

Tags


Marko maluli
Msanii Kitale amenaswa leo february 23 kwenye U-heard ya Soudy Brouwn ambapo amewachana Madee na Nay wa Mitego kuwa waache waache kujiita marais wa Manzese wakati Kimara……..
>>>”Ney wa mitego anakaa Kimara na Madeee anakaa kimara ndani kabisa, wanaongopea watu wa Mazese, wakiona tu wanataka kutoa nyimbo lazima watafute kiki zisizo kuwa na maana, mtu kama Nay kila siku akitaka kutoa nyimbo anazungumzia Bongo Muvie tu, Madee akitaka kutoa nyimbo mara utasikia kagombana na mtu Uingereza”
Kwa upande wake Nay wa mitego ameyasema haya……>>> Mimi hivyo vitu sivijui ninachojua nafanya muziki wangu na watu wangu, hao watu wengine wakiongea wanajua wenyewe, labda kaona Movie haziuzi kaona aje huku mwambie atoe single”
Kusikiliza Full story, Bonyeza play hapa chini 

MAOMBI KWA MANISPAA YA DODOMA MJINI JUU YA BARABARA YA BUKOBA STREET

Tags

Marko maluli

Manispaa ya Dodoma mjini mnaombwa muitengeneze Barabara hii ya Bukoba Street iliyopo Maeneo ya Uhindini..

Kiukweli barabara hii ni muhimu sana kwanza ni barabara inayo unganisha Nyerere Square na pia ndio njia kuu inayotumiwa na wapita kwa minguu.

Wikii hii yote Muungwana Blog imepokea malalamiko juu ya Barabara hiyo..

Wafanya Biashara na wakazi wa mtaa huo wanalalamika juu ya uchakavu wa Barabara hiyo ambayo ndio kiunganishi cha Nyerere Square na Sido.

Mnaombwa muirekebishe na kuiweka lami kama mitaa mingine ya hapo Uhindini.



Magazeti ya Tanzania February 23, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo

Tags


Marko maluli
Good Morning mtu wa nguvu, leo niFebruary 23 2017 na kama ilivyo kawaida yangu ya kila siku alfajiri nimekusogezea habari kubwa kwenye Magazeti kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia yaUdakuHardnews na Michezo ili uje kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu na blogs yangu


























ZITTO Kabwe Azidi Kuibana Serikali Kuhusu ufisadi wa IPTL....Amtaka Rais Magufuli Achukue Hatua

Tags



Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ameendelea kumtaka Rais Magufuli kuchukua hatua dhidi ya anachokiita ufisadi katika kampuni ya uzalishaji umeme ya IPTL, inayomilikiwa na Kampuni wa PAP.

Tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani mwezi Novemba mwaka 2015, Zitto amekuwa mstari wa mbele kumsihi na kumuomba Rais Magufuli afanye maamuzi juu ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikilipwa milioni 300 kila siku bila kujali kama inazalisha umeme au la.

Kupitia mitandao ya kijamii, Zitto ameandika "Rais John Magufuli ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa huu mtandao wa wizi na utapeli uliodumu toka mwaka 1995. watanzania masikini na wanyonge tutakuwa nyuma yake kwenye hili. Atende sasa."

Mnamo tarehe 21, Septemba 2016 Mhe. Zitto Kabwe alimtaka tena Rais Magufuli aoneshe hasira zake dhidi ya hicho anachokiita ufisadi mkongwe wa IPTL huku akieleza masikitiko yake juu ya kutochukuliwa kwa hatua zozote hadi sasa.

Mhe. Zitto Kabwe ambaye amekuwa hachoki kulizungumzia sakata hilo la IPTL amehoji ni nini kipo nyuma ya pazia, na ni nani mfaidika hadi hatua zisichukuliwe, huku akitoa ushauri wa hatua zinazoweza kuchukuliwa na mahakama kwa sasa.

"Mahakama Ina uwezo wa kurejea maamuzi yake kwa kuitisha upya kesi zilizoamuliwa. Hivi hii Mahakama haioni suala la PAP kumiliki IPTL na kuchota mabilioni ya fedha zilizokuwa Benki Kuu na kuendelea kulipwa tshs 300m kila siku izalishe au isizalishe umeme? Ushahidi wote ulionyesha utapeli wa Kimataifa uliofanywa na Harbinder Singh Seth lakini kivuli cha uamuzi wa Mahakama umefanya matapeli hawa kuendelea kunyonya fedha kutoka TANESCO. Huu mrija wa PAP/IPTL upo kinywani mwa The Chato Inc? Ama ni jipu la mgongoni?". Alihoji Mhe. Zitto Kabwe

Kichuyaaaaaaa: Tanzania 2 v DRC 0