Wednesday, March 7, 2018

UZURI WA SURA UENDANE NA USAFI WA MWILI

Tags


Image result for usafi wa mwili kwa mwanamke








Na MARKO MALULI
Imepakiwa-wednesday march 07-2018 at 20:02 PM
Habarini ndugu wasomaji wa makala hii ,leo naenda kuzungumzia wale marafiki zangu ambao muonekano wao wa nje ukiwaona ni nadhifu lakini ukiangalia ndani KAHARUFU (SMELL) KANAPENYEZA
Nywele
Iwapo nawe uko kwenye kundi hili, jiulize iwapo sisi wapita njia tunastushwa na harufu kali ya nywele zako, vipi mzee unayelala naye kitanda kimoja kila siku?

Mdomo
Halafu kuna wale wenye harufu mbaya mdomoni. Akifunua mdomo kuzungumza, lazima utageuza sura upande mwingine. Kwani ndani ya huo mdomo itatoka harufu ya samaki, sambusa, pilau na hata mahamri aliyokula jana ama  mchana. Kwa kifupi akina dada hawa hawajui kusafisha midomo hadi iwe shwari na iwe na harufu mwanana. Pamoja na kwamba harufu hii huwa ni dalili ya ugonjwa wakati mwingine wa mdomo, ni muhimu kujali usafi kabla ya kufikiria masuala ya kumwona daktari.

Kwapa
Kuna wale shoga zangu ambao wakipita mahali watu wote wanageuka, sio kwa kufurahia alivyoumbwa, bali harufu kali ya kwapa inayoambatana naye. Yaani wewe ukipita mahali, watu wanageuza shingo na wengine wanatema mate, kisa ni harufu ya kwapa lako. Naye mumeo hana amani nyumbani, labda anashindwa kukwambia kwamba harufu ya jasho lako ni mateso makubwa kwake. Usafi wa kwapa ni muhimu kila unapooga.

Sehemu nyeti
Mwanakwetu, sehemu nyeti inatakiwa iwe katika mandhari nzuri wakati wote. Ukienda kujisaidia haja ndogo, jipanguse ama jitawaze na maji safi. Isiwe ukitoa nguo ya ndani tu, mzee anakunja sura kutokana na harufu kali. Akimaliza raundi moja, hataki kurudisha daruga lake uwanjani. Kwani mazingira ya ikulu hayamvutii hata kidogo.

Miguu
Kuna wale shoga zangu ambao akivua viatu, chumba hakikaliki tena kutokana na harufu kali inyotoka miguuni. Jamani, hata kama umevaa viatu vya kubana miguu, nawa na ipanguse kabla ya kuingia kwa mwenyewe.
Hivyo ni vijimambo tu, vinavyohitaji utundu kidogo. Mbona wengine wanajitunza vizuri? Kinachokushinda wewe ni kipi?
Mtoto wa kike upitishe siku bila kuoga, nani atakutamani? Au uoge mara moja pekee kwa siku, hapo vipi?
Tena wanaume wengine walivyo wambea, akipita na kusikia harufu ya kutatanisha, breki ya kwanza kwa rafiki zake. Akawasimulie jinsi unavyotoa harufu mbaya na usivyovutia. Kama ni mumeo, basi jiandae, kwani atavumilia kwa kiasi fulani na akichoka, atatafuta kule kwenye mandhari nzuri, ambako atapata tulizo la moyo wake.
Mwanamke anahitaji kuwa msafi. Na dawa ya kuwa msafi ni kuoga mara kwa mara. Na kuhakikisha unanawa maji mengi na kujipangusa vizuri.
Pamoja na yote haya, hii isiwe tiketi kwako kakangu, kumnyanyasa mkeo sababu anatoa harufu zisizofurahisha. Badala ya kumbagua, kumtenga ama kumsimanga, jaribu kuzungumza naye kwa upendo kwa madhumuni ya kumsaidia kupata suluhisho.
Na kuuliza kwako kuwe na utaratibu. Sio unaropoka maneno ambayo unajua bayana yatamuumiza roho mwenzako. Ukiona kwamba ukimwuliza atachukia, tumia njia mbadala ambayo unaona itapunguza makali ya maudhi yake.


EmoticonEmoticon

Kichuyaaaaaaa: Tanzania 2 v DRC 0