Penda kutumia maji…..na siyo tissue!!!! Kutokana na wanawake kuwa na joto kali kutumia maji itasaidia kuondoa particles zote za mkojo pale unapojiswafisha….zingatia kutumia maji safi…..kuliko tissue ambazo zingine huwa laini mno…kwahiyo pale unapojisafisha…kuna chembechembe zingine hubaki na kusababisha muwasho….Pia hutoa harufu mbaya….mwilini!!! imagine unatoka jisaidia na unabaki na chembechembe……duuh inapunguza steam kwa mwenziyo pale mnapokuwa wote…..!!! nadhani nimeeleweka…
Usishinde na nguo ya ndani siku nzima!! Najua wengi tumeshazoea kukaa na nguo za ndani hata siku nzima…jamani kiafya haitakiwi….inashauriwa ubadilishe nguo ya ndani hata mara mbili au tatu kama ukiweza…tena hapo uifue na kuiloweka…..na uanike juani ili ikauke na mwanga na siyo upepo kama tulivyozoea……..
Usikae na pedi zaidi ya masaa matatu….. Tunapokuwa kwenye siku zetu….sijui ni ubahili au ulimbukeni…mi sielewi…mtu anaweza akashinda na pedi moja siku nzima….heee jamani ule ni uchfu unaotoka mwilini…unavyoshinda nao hivyo husababisha bacteria kutengenezwa ukeni…na kupata cancer ya kizazi…wanawake embu tufumbuke macho na kuwa wasafi jamani..huoni kama unakuwa na harufu mabaya mwilini????? au ni mazoea??? Kuwa msafi husaidia kuwa mrembo na hasa kuvutia na kujisikia huru mbele za watu…..Ukiwa katika siku zako, penda kujiswafisha mpaka ndani,,,hii itasaidia kupunguza siku za kuwa kwenye hedhi…kama huamini..basi jaribu…….!!! Kama ulikuwa unaingia mwezini kwa siku saba….zinaweza kupungua hata mpaka siku tatu…pale tuuu utakapojua kujiswafisha vizuri…na siku zilizobaki ukawa huru….
Tumia sabuni za kunukia….. Kuna wanawake wengine jamani wameumbwa kuwa na vikwapa vyenye harufu kali…siyo kosa lao….jamani lakini siku hizi kuna sabuni za kila aina ..basi jitahidi kutumia hizo ..au kuoga mara mbili kwa siku pia husaidia….tumia limao au ndimu pale unapooga kujisafisha makwapani… na sehemu zingine ambazo zimekakamaa kwa weusi wa kunyoa ……hii itasaidia kukata harufu mbaya na kuondoa ule weusi weusi sehemu hizo…….Unakuta mwanamke mzuuri, mrembo…but akinyanyua mkono loo…aibu tupu…jamani siku hizi kuna mpaka specialist wa ngozi kama imeshindikana basi nenda kawaone……
Kwa kumalizia tuu labda niseme….kwamba ukiwa msafi nje na hata ndani itakusaidia kuwa huru na mwenye furaha saa zote..huwezi kuwa unatoa harufu na ukawa na amani..au nadanganya??? please tujitahidi kufata hayo mambo niliyowaambia mzingatieeee……unakuta uko na mwenziyo mpaka anaona kero kukaa na wewe….inahusu jamani??? unamkatisha mwenziyo hamu kisa uchafu wako…..siyo lazima akwambie direct…lakini unaweza kujishtukia tuuu mtu hana mood tena ya kufanya tendo la ndoa…..!!!! ni hayo tuuuu………!!!!!
Mwandishi wenu Marko Maluli
Mwandishi wenu Marko Maluli
EmoticonEmoticon